HAWA WAKO KWENYE VITABU VYA KARIAKOO DABI

NGOMA inatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 20 2024 kwenye Kariakoo Dabi ambapo kila timu itakuwa kazini kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.
Ikumbukwe kwamba kwenye mzunguko wa kwanza mchezo uliochezwa Novemba 5 2023 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga.
Hawa hapa waliofunga Kariakoo Dabi tukianza na wenyeji Yanga namna hii:-

Kennedy Musonda
Mwamba aliyefungua pazia la kufunga alikuwa ni Musonda mapema dakika ya tatu alimtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.kariakoo dabiMaxi Nzengeli
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza mwamba alitupia jumla ya mabao mawili akiwa ni nyota aliyefunga mabao mengi zaidi katika mchezo huo na mpaka sasa kafuga jumla ya mabao 9 kwenye ligi.

Aziz KI

Kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi alifunga bao moja na mpaka sasa ana jumla ya mabao 14 kibindoni akiwa ni namba moja kwa mastaa wenye mabao mengi zaidi ndani ya Kariakoo Dabi.

PACOME

Pacome alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalti kwenye mchezo wa Karikoo Dabi akikamilisha bao la tano mbele ya Simba akiwa kafunga jumla ya mabao 7 kwenye ligi msimu wa 2023/24.kariakoo dabi

KIBU DENIS

Novemba 5 2023 ilikuwa chungu kwa Simba walipopoteza pointi tatu mazima, bao pekee la Simba lilifungwa na Kibu Dennis ambaye alikwama kukamilisha dakika 90 baada ya kupata maumivu kwenye mchezo huo.

Mpaka sasa Kibu ana bao moja pekee na katengeneza jumla ya pasi tatu za mabao ndani ya kikosi cha Simba kilichocheza mechi 20 na yeye alipata nafasi ya kucheza kwenye mechi 19.

Acha ujumbe