Kariakoo Dabi Kupigwa April 20

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imetoa tarehe rasmi ya mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira Tanzaniam Afrika Mashariki na hata Afrika kwa ujumla wakeambao unafahamika kama Kariakoo Dabi.

Kariakoo Dabi ni mchezo unaokutanisha mahasimu wawili wa mpira nchini Tanzania vilabu vya Simba na Yanga, Mchezo huu haukua unepangiwa tarehe rasmi ya kupigwa lakini bodi ya ligi imetoa tarehe rasmi leo na kusema mchezo huu utapigwa mwezi huu tarehe 20.kariakoo derbyVilabu hivi vinakwenda kukutana katika mchezo huu huku vyote vikiwa na vimetoka kutupwa nje kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, Ambapo wote wametokea kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Mchezo huu pia utakua ni kama wa kulipa kisasi kwa upande fulani kwani klabu ya Simba inaingia kwenye mchezo huu na kumbukumbu ya kilichotokea tarehe 5 Novemba mwaka jana, Ambapo walipokea kichapo kizito cha mabao matano kwa moja mbele ya mtani wake Yanga.kariakoo derbyKlabu ya Yanga wao kuelekea Kariakoo Dabi watakua wana mkakati mmoja tu nao ni kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC, Kwani watani zao Simba wanakuja kwa karibu na kutaka kuwania taji hilo ambalo Yanga wanataka kulitetea.

Acha ujumbe