SINGIDA FOUNTAIN GATE HAWAPOI

UONGOZI wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Future kutoka Misri.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 17 ikiwa ni hatua ya pili ya awali ya mashindano hayo.singida fountain gateOfisa Habari wa Singida, Hussein Masanza alisema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo wa kimataifa na maandalizi yapo vizuri.

“Tupo tayari kwa ajili ya mechi yetu ya kimataifa ambayo tutaanza hapa Azam Complex benchi la ufundi linafanya kazi kubwa kufanya maandalizi mazuri ambayo yataleta matokeo mazuri.singida fountain gate“Tunatambua ushindani ni mkubwa nasi tupo tayari kupata matokeo mazuri, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi ili tufanye vizuri kimataifa,” alisema Masanza

Acha ujumbe