
Usikuwa tuzo za TFF ulitamatika Juni 12, 2023 huko mkoani Tanga, huku klabu ya Simba na Yanga zikitambiana kwenye tuzo hizo. Macho na masikio ya wengi yalikuwa yakisubiri kuona tuzo ya mfungaji bora wa Ligi kuu inaenda kwa nani ikiwa Mayele wa Yanga na Saidoo Ntibazonkiza wa Simba wakifungana kwa mabao 17.
Tuzo za Azam Federation Cup
Golikipa Bora alikuwa ni Djigui Diarra wa Yanga Sc akiwatupa Benedict Haule wa Singida Big Stars na Abdulah Idrisu wa Azam FC. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Tuzo ya Mfungaji Bora ilikwenda kwa Andrew Simchimba wa Ihefu aliyefunga mabao saba.
Tuzo ya Mchezaji Bora ilikwenda kwa, Bakari Mwamnyeto akiwatupa Prince Dube na Abdul Sopu wa Azam na Clement Mzize wa Yanga.
Tuzo za Ligi Kuu
Tuzo ya Kocha Bora wa Msimu ilikwenda kwa Nasredin Nabi wa Yanga, akiwatupa, Roberto Oliveira wa Simba na Hans Van Plujim wa Singida Big Stars.
Tuzo ya Fair Play ilikwenda kwa Saido Ntibazonkiza, akiwatupa Jean Baleke wa Simba na Pape Osman Sakho.
Tuzo ya Chipukizi Bora ilikwenda kwa Lameck Lawi, akiwatupa Clement Mzize wa Yanga, Edmund John wa Geita Gold FC. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Tuzo ya Beki Bora ilikwenda kwa Dickson Job, akipokea kijiti kutoka kwa Henock Inonga wa Simba Queens akiwatupa pia, Bakari Nondo wa Yanga, Shomari Kapombe wa Simba na Mohamed Hussein wa Simba.
Tuzo ya Kiungo Bora ilikwenda kwa Saidoo Ntibazonkiza, akiwacha Bruno Gomes wa Singida Big Stars, Azizi Ki wa Yanga, Clatous Chama na Mzamiru Yasini wa Simba.
Golikipa Bora wa Msimu ilikwenda kwa Djigui Diarra wa Yanga, akiwatupa Aishi Manula wa Simba, Benedict Haule wa Singida Big Stars.
Tuzo ya Mfungaji Bora wa Msimu ambayo ilikuwa imezua utata. Ndipo kamati ilikaa na kuamua kuwapa Fiston Mayele na Saidoo Ntibazonkiza wa Simba wote kiatu cha dhahabu wakiwa na mabao 17.

Tuzo ya Goli Bora la msimu ilikwenda kwa Fiston Mayele wa Yanga, akiwatupa Hamad Majimengi Elias Maguli wa Geita Gold FC, Charles Ilafya wa Mtibwa Sugar na Stephan Azizi Ki.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) ilikwenda kwa Fiston Mayele akiwatupa Mzamiru Yasin wa Simba, Bruno Gomes wa Singida Big Stars, Djigui Diarra wa Yanga na Saidoo Ntibazonkiza wa Simba.
Kikosi Bora Cha Msimu wa NBC, Djigui Diarra wa Yanga, Shomari Kapombe – Simba, Mohamed Hussein, Simba, Dickson Job Yanga. Bakari Mwamnyeto – Yanga, Hennock Inonga Simba.
Mzamiru Yassin Simba, Bruno Gomes Singida BS, Fiston Mayele Yanga, Clatous Chama Simba na Saidi Ntibazonkiza. Kocha Bora wa NBC alikuwa ni Nasredin Nabi, akiwatuoa Roberto Olivieira wa Simba na Hans Van Plujim wa Singida.
Timu yenye nidhamu ni KMC ya Dar, tuzo ya heshima ilikwenda kwa Rais Samia Suluhu kutoka wa Rais wa TFF Wallace Karia. Mchezaji Bora Championship ni Edward Songo wa JKT Tanzania.
Mchezaji Bora wa First League ni Tungu Kashinje wa Stand United. Tuzo ya Mchezaji Gwiji ilikwenda kwa Leopod Mukebezi. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

