Shirikisho la Soka Uganda FUFA lipo kwenye mazungumzo ya kutaka kumpa kazi Kocha wa Simba Queens Charles Ayiekho kuinoa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Uganda (Crested Cranes). Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.
Kocha huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa mwaka jana akicheza fainali ya Cecafa kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba akiwa na She-Corporate ya kwao Uganda na kupoteza kwa bao 1-0.
Anapewa timu hiyo ya taifa Ili apambane kusaka tiketi ya kwenda Olimpiki 2024 huko Paris Ufaransa na kuisimamia kwenye mechi nyingine za kufuzu Kombe la Dunia na mashindano ya Afrika. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Uganda hawakuwa na kocha mkuu tangu Julai mwaka jana baada ya George Lutaro kuondoka kwenye timu hiyo baada ya kushindwa kufuzu kwenda mashindano ya Afrika kwa wanawake (AWCON) iliyofanyika mwaka Jana nchini Morocco.
Taarifa kubwa kutoka ndani ya Simba Queens zinasema kocha huyo ameshabwagana na Simba Queens na hiyo imekuwa tiketi yake ya kuachana na Simba Queens ambayo hajamaliza nayo msimu vizuri. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Alipotafutwa Ayiekho mwenyewe kwa njia ya simu. Bahati mbaya hakuweza kuthibitisha kuwa ni kweli amesema mazima au atarudi. Kadhalika kwa upande wa Simba picha ilikuwa hivyo pia. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.


