Taifa Stars Kutafuta Tiketi ya Afcon leo Dhidi ya Uganda

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars leo itashuka dimbani kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika Affon mwakani nchini Ivory Coast dhidi ya timu ya taifa ya Uganda katika dimba la Benjamin Mkapa.

Taifa Stars walifanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa bila katika mchezo uliopigwa wiki iliyomazika nchini Misri siku ya Ijumaa, Hivo wataendelea kupambana katika mchezo wa leo ili kupata alama tatu muhimu ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu michuano ya Afcon.Taifa starsTimu ya taifa ya Tanzania ilifuzu michuano ya Afcon mwaka 2019 lakini mwaka huu wanaonekana wako kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwani wanahitaji alama nne kwenye michezo miwili kufuzu, Hiii ikimaanisha wakishinda dhidi ya Uganda leo watahitaji sare dhidi ya Niger mchezo wa mwisho.

Taifa Stars wakiwa chini ya mwalimu Amrouche wameongeza wachezaji wawili kwenye kikosi hicho ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho dhidi ya Uganda leo, Ambao ni mabeki wa klabu ya Simba Mohamed Hussein na Shomari Kapombe ambao waliachwa kwenye mchezo wa kwanza.Taifa starsTaifa Stars leo itakua na faida ya kucheza katika uwanja wake wa nyumbani ambao utakua na mashabiki wa klabu hiyo wakiipa hamasa timu hiyo katika mchezo huo, Lakini pia mchezo wa mwisho ambao utaamua hatma yao kuelekea Afcon pia utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.