Conte Awashukuru Mashabiki Spurs

Aliyekua kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs raia wa kimataifa wa Italia Antonio Conte amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuachana na klabu hiyo mapema siku ya jumapili.

Antonio Conte ambaye amedumu ndani ya klabu ya Tottenham amefanikiwa kukaa ndani ya klabu hiyo kwa takrinani mwaka mmoja na nusu, Lakini ameishia kuachana na klabnu hiyo baada ya kutofurahishwa na mwenendo wa klabu hiyo kuanzia kwa wachezaji mpaka uongozi wa klabu hiyo.ConteKocha alikua mwenye hasira kali baada ya klabu ya Tottenham kusawazishiwa mabao katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Southampton na mchezo kuisha kwa mabao matatu kwa matatu, Kitu kilichomfanya kocha kuwatupia lawama wachezaji wa klabu hiyo na kusema wachezaji hao hawajitumi.

Kocha Conte aliwatuhumu wachezaji wa klabu ya Tottenham na kusema kua wachezaji hao hawajitumi na ni wabinafsi, Vilevile sio wachezaji ambao wanacheza kwajili ya kuipigania kalbu hiyo hivo kumfanya kocha huyo kuamua kuachana na timu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.ConteAntonio Conte baada ya kuachana na klabu ya Tottenham inaelezwa yuko mbioni kurejea ndani ya klabu ya Inter Milan, Kwani Inter Milan wanaelezwa wako kwenye mchakato wa kumtimu mwalimu wao wasasa Simeone Inzaghi ambaye inaonekana ameshindwa kuipa mafanikio timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.