Conte Atema Nyongo Spurs

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs raia wa kimataifa wa Italia Antonio Conte ameamua kutema nyongo baada ya klabu ya Tottenham kutoka sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Southhampton.

Kocha Conte alioneshwa kutokufurahishwa na kitendo kilichotokea katika mchezo wa jana na kalbu yake kudondosha alama mbili wakiwa katika dimba lao la nyumbani, Kocha huyo anasema klabu hiyo imeklua na wachezaji wasiotaka kujituma kwa muda mrefu na ndio sababu kubwa ya matokeo ya mabaya.ConteKocha huyo raia wa Italia anasema klabu hiyo imekua namatokeo hayohayo kwa miaka 20 sasa na imekua haijalishi kocha ambae anakuja, Lakini hali imekua haibadiliki ndani ya timu hiyo na wachezaji wa timu hiyo wamekua wakiwaangusha mashabiki wa klabu hiyo kutokana na mwenendo wao.

Conte anasema amepita klabu kadhaa lakini hajakuwahi kukutana na wachezaji wa aina ya Spurs kwani wachezaji wa klabu hiyo wamekua wabinafsi, Amesema wachezaji wa klabu hiyo hawachezi kwasababu ya klabu hiyo bali kila mchezaji anaingia uwanjani kwajili yake na sio timu kwa maana ya ubinafsi wa kupitiliza.ConteKocha Conte anaeleza amekua akivumilia hali hiyo kwa muda lakini kwasasa hawezi kukaaa kimya tena, Kwani hali inaendelea kua mbaya zaidi kutoka msimu uliomalizika mpaka sasa huku akiongeza kua wachezaji hao hawataki kucheza kwa presha wala kuwaza kupiginia kitu wao wanataka kucheza bila kupambana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.