Taarifa zinaeleza kua kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs raia wa kimataifa wa Italia Antonio Conte anajipanga kurejea ndani ya klabu ya Inter Milan ambapo aliondoka kabla ya kujiunga na Tottenham.

Kocha Conte inaelezwa yupo kwenye mipango ya kuachana na klabu ya Tottenham mwishoni mwa msimu huu na kurejea ndani ya wababe wa Italia klabu ya Inter Milan ambapo alitwaa taji la ligi kuu ya Italia mara ya mwisho alipokua akifundisha ndani ya klabu hiyo.conteKlabu ya Inter Milan pia inaelezwa ipo kwenye mchakato wa kumtimua kocha wake wasasa Simeone Inzaghi ili ampishe Conte katika nafasi hiyo, Kwani mabosi wa klabu hiyo hawafurahishwi na muenendo wa klabu hiyo chini ya kocha Inzaghi haswa kwenye ligi kuu ya Italia ambapo imekua ikipata matokeo ya kusuasua.

Klabu ya Tottenham wenyewe inaelezwa wanataka kocha huyo ahakikishe wanamaliza nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini kama atashindwa basi watamtimua na haitajalisha kama atakwenda Inter Milan au la kwani mipango ya klabu hiyo ni kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.conteAntonio Conte amekua hana msimu mzuri ndani ya klabu ya Tottenham msimu huu hivo inawezekana kimbilio lake na yeye limekua ni kurudi katika ligi ya nyumbani ambapo amekua akifanya vizuri, Kwani ameshafanikiwa kubeba taji la ligi nchini humo na vilabu viwili tofauti ambavyo ni klabu ya Juventus na Inter Milan.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa