Lukaku anatarajiwa Kurejea Chelsea

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea anayekipiga kwa mkpo klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku anatarajiwa kurejea ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake wa mkpo kumalizika.

Romelu Lukaku alipelekwa kwa mkopo klabu ya Inter Milan baada ya kushindwa kuingia kwenye mfumo wa aliyekua kocha wa klabu hiyo Thomas Tuchel, Hivo kupelekea mchezaji huyo kutolewa kwa mkopo kuelekea klabu ya Inter Milan kwa msimu mzima.LukakuMshambuliaji huyo alitarajiwa kununuliwa kwa mkataba wa kudumu ndani ya Inter Milan kwani alishacheza hapo kwa kiwango cha juu, Lakini kauli ya mkurugenzi wa klabu hiyo imeibua utata kwani na kuonesha huenda mchezaji huyo hayupo kwenye mipango yao tena na atarejea kwenye klabu yake ya Chelsea.

Mkurugenzi wa Inter Milan Beppe Marotta amesema kua nyota Romelu Lukaku bado hajarudi kwenye utimamu wake ambao wamekua wakiufahamu, Kupitia kauli hii ni wazi mkurugenzi huyo hajavutiwa na kiwango ambacho ameonesha mshambuliaji huyo mpaka sasa ndani ya klabu hiyo.LukakuTangu Lukaku arudi Inter Milan kwa mara nyingine amekua akiandamwa na majeraha kitu kilichomfanya kushindwa kuitumikia klabu hiyo mara kwa mara, Hii imepelekea pia mshambuliaji huyo kushindwa kuonesha ubora wake ndani ya klabu hiyo na kufanya waajiri wake wasasa kupiga chini mpango wa kumnunua jumla.

Acha ujumbe