Kocha wa klabu ya Inter Milan Simeone Inzaghi amepomgeza umoja wa timu yake baada ya kupata matokeo ya ushindi dhidi ya klabu ya Fc Porto katika mchezo wa hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa ulaya usiku wa jana.
Kocha Inzaghi amefurahishwa na mchezo mzuri ambao umeoneshwa na vijana wake katika mchezo dhidi ya Fc Porto wakiwa ugenini katika dimba la Dragao, Kocha akisema timu yake ilifanikiwa kupata matokeo mazuri baada ya kua na umoja wakiwa kiwanjani na kuhakikisha wanasonga mbele kwenye michuano hiyo.Klabu ya Inter Milan jana imefanikiwa kuitupa nje klabu ya Fc Porto baada ya kulazimisha sare tya bila kufungana katika mchezo huo, Huku Inter Milan wakiwa na faida ya bao moja ambalo walishinda katika dimba lao la nyumbani San Siro wiki kadhaa nyuma na kuwahakikishia kufuzu hatua ya Robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.
Kocha Inzaghi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo alieleza kua mpira wa miguu ni mchezo wa bahati, Lakini klabu yake ilistahili kufuzu hatua ya Robo fainali na hiyo inatokana na ubora ambao waliuonesha katika mchezo kuzuia kwa ushirikiano mkubwa ndio siri ya mafanikio yao.Klabu ya Inter Milan imekua na miaka mingi ikishindwa kufuzu hatua ya Robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya lakini kupitia kocha Simeone Inzaghi wamefanikiwa kutinga hatua hiyo, Vilevile kiungo wa klabu hiyo Henrik Mikhytaryan amewapongeza wachezaji wenzake baada ya kufuzu hatua hiyo iliyokosekana klabuni hapo.