Klabu ya Tottenham Hotspurs imepanga kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane wakati huu mkataba mpya wa mshambuliaji ukielekea ukingoni.
Klabu ya Tottenham bado imeendelea kuonesha inahitaji huduma ya nyota huyo ambaye tayari amekua mfungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo, Klabu hiyo inataka kumuongezea mkataba Kane licha ya nyota huyo kuhitajika na vilabu kadhaa barani ulaya.Harry Kane ameendelea kua na msimu bora kama ilivyo kawaida yake akiwa tayari ameshafunga mabao 20 kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa nyuma ya Haaland kwa mabao 8, Ubora wake umeifanya klabu yake kufikiria kuendelea kusalia na nyota huyo.
Mkataba wa Harry Kane unamalizika Juni mwaka 2024 ni wazi mshambuliaji huyo amebakiza mwaka mmoja wa kutumikia klabu hiyo, Hali hii inaiweka klabu ya Tottenham kwenye wakati mgumu kwani nyota huyo asipoongeza mkataba mpya ana nafasi kubwa ya kuondoka bure baada ya mkataba wake kumalzika.Taarifa zinaeleza kua klabu ya Tottenham inapanga kumuongezea mkataba mchezaji huyo lakini ikiwa haijaondoa uwezekano wa kumuuza kwa klabu ambayo itafika dau ambalo wameliweka, Huku Manchester United inaelezwa imepanga kumfanya Kane kua mchezaji ghali kabisa wa kiingereza ndani ya klabu hiyo.