Kiungo wa klabu ya Simba Clatous Chama amefanikiwa kuchaguliwa kua mchezaji bora wa wiki wa michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya raundi ya nne ya michuano hiyo kumalizika.

Chama alikua akiwania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wengine kama Ahmed Zizo kutoka klabu ya Zamalek, Peter Shalulile kutoka Mamelodi Sundowns, na Walid Sabbar kutoka Raja Casablanca lakini kiungo huyo wa Wekundu wa Msimbazi amefanikiwa kushinda.chamaKiungo Clatous Chama amefanikiwa kushinda kinyang’anyiro hicho akiwashinda wenzake wote kutokana na idadi ya kura ambazo amezipata mbele ya wachezaji wenzake, Hii inakua mara ya kwanza kwa kiungo huyo kushinda kinyang’anyiro cha kua mchezaji bora wa wiki wa michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.

Chama amefanikiwa kushinda baada ya kuonesha kiwango bora sana katika mchezo dhidi ya Vipers United ya nchini Uganda katika uwanja wa taifa jijini Dar-es-Salam katikati ya wiki iliyomalizika,Kiungo huyo alifanikiwa kufunga bao pekee ambalo liliwapa klabu ya Simba alama tatu muhimu.chamaKiungo huyo wa kimataifa wa Zambia amekua akifanya vizuri ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu sasa na kumfanya kua moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Simba, Lakini pia kiungo huyo ameingia ndani ya kikosi bora cha wiki cha michuano ya ligi ya mabingwa Afrika zaidi ya mara moja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa