Kiungo wa klabu ya soka ya Simba Clatous Chama atawakosa klabu ya soka ya Dodoma jiji kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa siku ya jumapili jijini Dodoma.
Kiungo fundi Clatous Chama taarifa zinaeleza kua mchezaji huyo alipata majeraha katika mazoezi ya mwisho ya klabu hiyo kabla ya kusafiri kuelekea jijini Dodoma. Hivo kutokana na majeraha hayo yatamfanya mchezaji huyo kuwakosa klabu ya Dodoma Jiji.Kiungo huyo wa kimataifa wa Zambia hajasafiri na timu kuelekea jijini Dodoma ambapo ndipo mchezo huo utakapopigwa katika uwanja wa Jamhuri. Kutokana na kiungo huyo kutokusafiri na klabu ya Simba kuelekea jijini Dodoma ni wazi hatakuepo katika mchezo huo.
Kiungo huyo Chama ambaye ndio mchezaji anayeongoza kwa kupiga pasi za mwisho katika ligi kuu ya NBC kukosekana kwake katika mchezo huo kunaacha pengo kubwa ambalo mara nyingi linaieweka Simba kwenye wakati mgumu. Kocha Robertinho ana kazi ya kufanya kuhakikisha anaweza kuziba pengo la mchezaji huyo na kuweza kupata alama tatu muhimu.Mbali na mchezaji Clatous Chama kukosekana katika mchezo huo lakini pia klabu ya Simba itawakosa nyota wake watatu katika mchezo huo ambao watakua wanatumikia adhabu, Ma nyota hao ni viungo wawili Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute, Pamoja na beki Joash Onyango ambao walipata kadi tatu za njano.