Tchouameni Aomba Radhi Real Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Aurelien Tchouameni ameiomba radhi klabu yake ya Real Madrid kutokana na kitendo chake cha kuhudhuria mchezo wa kikapu jijini Paris.

Kiungo Tchouameni alihudhuria mchezo wa kikapu uliopigwa jijini Paris kati ya Chicago Bulls na Detroit Pistons huku klabu yake ya Real Madrid ikiwa na mchezo wa kombe la Copa De Le Rey dhidi ya klabu ya Villarreal ndio sababu iliomfanya aombe radhi kwa klabu yake.TchouameniKiungo Tchouameni alitumia mitandao yake ya kijamii kuomba radhi kwa kuandika “Naomba radhi kwa klabu yangu, timu ya wakufunzi, wchezaji wenzangu na mashabiki wa Real Madrid kwa uwepo wangu kwenye hafla wakati timu yangu ipo kwenye mchezo. Nimekua makini kwa kila kilichokua kikitokea Villarreal lakini sijafanya jambo sahihi samahani sana”

Kiungo huo ameomba radhi ikiwa amejua jambo alilolifanya sio sahihi kwani alisafiri kutoka jijini Madrid na kuelekea jijini Paris kuangalia mchezo wa mpira wa kikapu wakati alipaswa kubaki jijini Madrid au kusafiri na timu kwajili ya kutoa ushirikiano kwa wachezaji wenzake.TchouameniKiungo Aurelien Tchouameni amekua kwenye majeraha kwa wiki kadhaa sasa ambapo ndio sababu iliyompa wepesi wa kusafiri na kwenda nchini Ufaransa kuhudhudria mchezo wa kikapu, Lakini mchezaji huyo ametambua makosa yake na ameomba radhi kwa klabu yake ya Real Madrid jambo ambalo limetafsiriwa kama la kiungwana zaidi.

Acha ujumbe