Timu ya taifa ya mpira wa miguu Tanzania Taifa Stars imefanikiwa kupata kocha mkuu rasmi raia wa kimataifa wa Algeria akifahamika kama Adel Amrouche mwenye umri wa miaka 58.
Taifa Stars ambayo ilikua haina kocha kwa muda mrefu sasa lakini kuanzia leo kocha Adel Amrouche atakiongoza kikosi cha Tanzania kwa muda ambao haujawekwa wazi na shirikisho la soka Tanzania(TFF) lakini kocha huyo anaelezwa kua na uzoefu mkubwa sana.Shirikisho la soka Tanzania limempa kibarua kocha huyo ambaye amefanikiwa kufanya kazi sehemu tofauti tofauti hapa barani Afrika akivifundisha vilabu Dc Motema Pembe ya Congo, USM Alger ya nchini kwao Algeria na vilabu vingine mbalimbali .
Kocha Adel Amrouche pia amewahi kufuindisha timu mbalimbali za taifa kama Yemen, Libya,Equatorial Guinne, Bostwana, na timu ya taifa ya Kenya ambayo alifanikiwa kuiongoza timu kucheza michezo ishirini bila kupoteza ikiwa ni rekodi nzuri zaidi kwa kocha huyo akiwa na timu ya taifa.TFF imeamua kumuajiri kocha Adel Amrouche raia wa kimataifa wa Algeria baada ya kumuona ni kocha sahihi kuifundisha Taifa Stars kutokana na uzoefu wake wa soka barani Afrika, Kwani kocha Amrouche ana uzoefu na soka la ngazi ya klabuni lakini pia vilevile ana uzoefu na soka la ngazi ya timu ya taifa.