Klabu ya Newcastle United imekua na bahati mbaya na timu kutoka katika jiji la Manchester kwani leo tena wamepokea kichapo kutoka klabu ya Manchester City katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Etihad.

Klabu ya Newcastle imekubali kipigo cha pili mfululizo baada ya kuchapwa na Man United wikiendi iliyomalizika katika mchezo wa fainali ya kombe la Carabao, Huku leo Manchester City wakifanikiwa kuifunga klabu hiyo kw mabao mawili kwa bila.manchester cityMabao ya Phil Foden na Bernardo Silva alietokea nje yaliwawezesha vijana hao wa Pep Guardiola kuweza kupata ushindi wa pili mfululizo baada ya kuifunga klabu ya Bournamouth kwa mabao manne kwa bila wikiendi iliyomalizika na leo wameendeleza wimbi lao la ushindi.

Klabu ya Manchester City wamefanikiwa kufikisha alama 58 wakiwa nyuma kwa alama 2 dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal, Huku Arsenal wao wakiwa na mchezo wao ambao wanatarajiwa kucheza dhidi ya Afc Bournamouth jioni ya leo.manchester cityManchester City bado wana matumaini ya kuweza kutetea taji lao kwani bado wana michezo mingi licha ya klabu ya Arsenal kuonekana kua kwenye ubora mkubwa msimu huu, Klabu ya Manchester City wanaonekana kuanza kurudisha ubora wao katika michezo yao waliyocheza siku za karibuni.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa