Allegri: Kuingia Nafasi ya nne kama tumebeba makombe matatu

Kocha wa klabu ya Juventus Massilimiano Allegri amesema wakifanikiwa kuingia kwenye nafasi nne za juu ambazi zitawafanya kufuzu ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao watafurahie kama wamebeba mataji matatu.

Klabu ya Juventus imepitia kipindi kigumu miezi kadhaa nyuma baada ya kukatwa alama 15 baada ya kubainika walifanya udanganyifu wa matumizi ya pesa, Hivo kuwafanya kushuka katika msimamo wa ligi hiyo kitu kinachomfanya Allegri aone kufuzu ligi ya mabingwa ni mafanikio makubwa saba kwao.allegriKocha Allegri anasema anajua ugumu uliopo kwa klabu yake kufuzu ligi ya mabingwa ulaya msimu huu, Lakini ni kitu ambacho anaona kinawezekana klabu ya Juventus kwasasa ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A wakiwa na alama zao 35.

Klabu ya Juventus wanahitaji kufanya kazi kubwa sana ili kuweza kumaliza kwenye nafasi nne za juu  katika msimamo wa ligi kuu ya Italia Serie A, Kwani vilabu ambavyo vipo juu yao pia vinaonesha ushindani mkubwa katika kuzitaka nafasi nne za juu na kuweza kufuzu michuano ya ulaya.allegriKocha Allegri wakati anaulizwa na wanahabari ataona kumaliza nafasi nne za juu kama kubeba taji la Serie A na kocha huyo kujibu ni kama watakua wamebeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja, Hii inaonesha namna gani itakua na ukubwa klabu hiyo ikifanikiwa kumaliza katika nafasi nne za juu.

Acha ujumbe