Taifa Stars Dimbani Leo dhidi ya Madagascar.

 

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ jioni ya leo itashuka uwanjani Madagascar katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia.

 

Mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri, ni wa kukamilisha ratiba kwani timu zote (Madagascar na Taifa Stars) zimeshaondoshwa mashindanoni.

Benin na DR Congo zitachuana katika mchezo mwingine ambao utaamua ni timu ipi inavuka raundi ya tatu majira ya usiku wa leo. DR Congo wanahitaji ushindi wakati Benin wanahitaji alama moja tu katika mchezo huo utakaopigwa Lubumbashi DR Congo.

Tanzania ilitua Madagascar juzi wakisafiri na ndege binafsi (ATCL) ambayo itawarudisha nyumbani baada ya mchezo huo.

Kumekuwa na taarifa kuhusu wanajeshi wa Madagascar kuzingira hoteli iliyofikia ya timu ya Taifa Stars, wakitaka kuchukua baadahi ya wachezaji kwa kuwatuhumu wana maambukizi ya virusi vya corona.


NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe