Jose Mourinho siyo tatizo kwenye klabu ya AS Roma, na klabu na mashabiki kwa pamoja wanapaswa kumuunga mkono. Kwa mujibu wa Francesco Totti
Roma walimteua Mourinho kuwa meneja mwezi Mei, na waliwekeza takribani €130m kwa ajili ya wachezaji wapya.
Licha ya mambo kuanza vyema, Roma wakishinda mechi zao sita za msimu kwa mara ya tatu kwenye historia yao, wameshinda mechi nne pekee katika mechi 12 walizocheza ugenini.

Baada ya hapo fomu ya Roma ikaanza kuporomoka na wakimaliza safari yao ya ushindi wa mechi 43 mfululizo za nyumbani .Mwezi Novemba pia haujawa mwema sana kwa Roma wakianza na kutoa sare nyumbani dhidi ya Bodo, kabla ya kukubali kichapo cha 3-2 dhidi ya Venezia.
“Kama tukidhani tatizo la Roma ni Mourinho, inamaanisha kila kitu hakiko sawa kwetu. Saluti kwa Mourinho, ameshinda mechi nyingi zaidi ukifananisha na mameneja wengine wote wa Serie A. Klabu na mashabiki wanapaswa kumuunga mkono”
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


