Kiungo wa crystal Palace Conor Gallagher ameitwa kwenye kikosi cha Uingereza kwa mara ya kwanza na anatarajia kuwepo kwenye mchezo wa kesho jumatatu dhidi ya San Marino kwenye mchezo wa mwisho kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar.
Conor Gallagher mwenye umri wa miaka 21 aliachwa kwenye mchezo wa juzi ijumaa ambao Uingereza ilishinda goli 5-0 dhidi ya Albania. Japo alikuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu alichokionyesha kwenye timu yake ya Crystal Palace.

Pia chama cha soka Uingereza kimetoa taarifa ya kuwaacha wachezaji watano kwenye mchezo wa kesho dhidi ya San Marino wachezaji hao ni Jack Grealish, Raheem Sterling, Luke Shaw, Jordan Henderson na Mason Mount.
Gallagher leo atajiunga na timu kwenye uwanja wa Tottenham Hotspur wa mazaoezi kabla ya kusafili kesho jumatatu kwenda San Marino kwa ajiri ya mchezo wao wa mwisho wa kufuzu kombe la Dunia.

Conor Gallagher ambaye yuko kwa mkopo Crystal Palace akitokea Chelsea kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kunaonesha kuwa na msimu mzuri mpaka sasa akiwa na Palace na akipewa muda anaweza kuwa ni moja ya viungo wazuri.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


