Baada ya Simba Queens kushindwa kupata nafasi ya tatu kwenye michuano ya Klabu bingwa kwa upande wa wanawake kocha Mkuu wa kikosi hicho, Charles Lukula amefunguka.

Lukula amesema kuwa tatizo kubwa ambalo wanakumbana nalo kwa sasa ni eneo la ushambuliaji la timu hiyo kuwa butu.

“Tumeshindwa kutimiza malengo yetu ya kupata angalau nafasi ya tatu kwenye mashindano haya lakini tumejifunza vingi kwani ni mara ya kwanza kwetu.

 

“Oppah ni mchezaji mzuri lakini katika eneo la ushambuliaji tunakosa mabao mengi hivyo tunapaswa kupata mshambuliaji mwenye mbio nyingi na akili.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa