Kocha Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula amesema kuwa licha ya kufungwa na Mamelodi Sundowns lakini anawapongeza wachezaji wake kutokana na viwango walivyoonyesha.

Simba Queens walipoteza mchezo wao wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya Klabu bingwa kwa upande wa wanawake jana baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mamelod Sundowns.


Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Lukula alisema: “Nawapongeza sana wachezaji wangu kutokana na viwango walivyoonyesha japo naweza kusema bahati haikuwa kwetu.

“Naweza kusema refa pia hakuwa upande wetu kwani tulipokuwa tunacheza faulo yeye alituadhibu kwa kadi ila kwa wenzetu aliwaambia msirudie.

“Kwa sasa tunaenda kujiandaa kwa ajili ya kupambania nafasi ya tatu hivyo nina imani tutarejea nyumbani na medali.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa