Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwapa sapoti wachezaji na benchi la ufundi hata katika kipindi kigumu.

Kaze amezungumza hayo baada ya timu hiyo kufanikiwa kuvuka katika hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho barani Afrika.

Kaze, Kaze: Tuisapoti Timu Kwenye Kipindi Kigumu, Meridianbet

Kaze alisema kuwa: “Niliongea baada ya mchezo wa kwanza kumalizika Dar kuwa tuna dakika 90 nyingine ugenini lakini watu walijua tunatolewa.

“Tuliwaona kwenye mchezo wa nyumbani walikuja na mbinu ya kuzuia tu na tulijua katika mchezo wa marudiano watakuja kwa lengo la kushambulia hivyo sisi tulikuja na mpango wetu.

“Tunawaomba wapenzi na mashabiki wetu wawe na timu tukiwa kwenye wakati mgumu kwa ajili ya kutusapoti.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa