Baada ya kutoka suluhu kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano dhidi ya Club Africain ya nchini Tunisia, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema bado nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ipo.
Mchezo huo wa michuano ya Shirikisho ulipigwa jana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Yanga wanapaswa kupata sare ya kufungana kwenye mchezo wa marudiano ili kupata nafasi ya kufuzu makundi.

Kaze alisema kuwa “Wachezaji wamejitahidi, wamefanya kila linalowezekana kupata ushindi lakini haikuwezekana hivyo kuna baadhi ya vitu vidogo vya kurekebisha.
“Ni ngumu kucheza na timu ambayo ina wachezaji tisa nyuma kwa mshambuliaji mmoja lakini tunajua kwenye mchezo wa marudiano hawatacheza hivyo wataenda kufunguka.
“Mimi naamini kwamba mchezo bado ni nusu nusu tunaenda kucheza ugenini lakini bado tuna nafasi ya kufuzu kwani tumemuona mpinzani wetu jinsi anavyocheza hivyo kuna kitu cha kufanya kwenye dakika 90 ambazo zimebaki.”

