Kocha Msaidizi wa klabu ya Yanga Cedric Kaze amesema wanakwenda kuchez kila mchezo wakiwa na malengo. Ameyazungumza hayo akiwa anafanya mahojiano na wanahabri kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya GEita Gold.

Kesho klabu ya Yanga itakua dimbani kucheza na klabu ya Geita Gold kutoka mkoani shinyanga katika mchezo utakaopigwa katika dimba la CCM kirumba jijini Mwanza.kazeKocha Kaze amesema “Tunaingia kwenye kila mechi kwa malengo hatuingii kwenye mechi kwa sababu ya kuendeleza takwimu ya kucheza bila kupoteza maana unaweza usipoteze lakini ukakosa kutimiza malengo ya Klabu. Kwetu sisi kitu kikubwa na malengo yetu ni kupata alama 3 kwenye kila mchezo”

Pia kocha huyo amefunguka kuhusiana na ratiba ilivyokua ngumu ndio maana wanafanya mabadiliko ya wachezaji ndani ya timu ““Tukicheza mchezo wa kesho tunakuwa tumecheza mechi nne ndani siku kumi, hakuna mwili wa binadamu unaweza kuhimili hili na ndio maana mnaona baadhi ya michezo tunafanya mabadiliko lakini tunahakikisha hayaathiri utendaji na malengo kwenye kipindi hiki kigumu.kazeHii imeonekana katika mchezo uliopita dhidi ya KMC ambapo klabu ya Yanga ilipumzisha baadhi ya wachezaji wake kwenye huo ambapo Yanga walipata ushindi wa bao moja kwa bila. Hii inaonesha umuhimu wa kua na kikosi kipana ili ratiba ikiwa ngumu unaweza kupumzisha baadhi ya wachezaji na wakacheza wengine.

Pia kocha Kaze amesisitiza Geita ni klabu nzuri na ina ina wachezaji wazuri, Hivo sio mechi rahisi lakini wao wanaenda wakiwatambua hilo na kwa ari kubwa lengo kupata alama tatu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa