Golikipa wa Manchester United David de Gea ametemwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Hispania kilichoitwa. Kikosi hicho ambacho kinajumuisha wachezaji 55 lakini golikipa huyo amekua sio miongoni mwao.

Golikipa huyo ambaye amekua kwenye kiwango bora kwa muongo sasa, Amekua hana uhakika wa nafasi katika timu hiyo tangu kocha wasasa Luis Enrique akabidhiwe timu hiyo.de geaKikosi cha wachezaji 55 cha awali ambacho huitwa hua kinatoa taswira halisi ya ni wachezaji gani mwalimu ana mpango nao. Hivo kuachwa kwa De gea kwenye kikosi cha awali kabisa kinatoa taswira mbaya kwa golikipa huyo.

 

Mwalimu Luis Enrique wa timu ya taifa Hispania amekua muumini wa magolikipa wenye uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi, Kitu ambacho kimekua kikimsumbua golikipa huyo wa Manchester United.

Golikipa huyo pia amekua akinyooshewa vidole hata kwenye klabu yake licha ya uwezo wake mkubwa wa kuzuia mashuti, Lakini uwezo wake hafifu akiwa na mpira mguuni imekua tatizo na watu kuamini ni golikipa aliepitwa na wakati.de geaDe gea ambaye mara ya mwisho kuitumikia timu hiyo kwenye michuano mikubwa ilikua michuano ya Euro 2020. Huku nafasi ya golikipa huyo ikisemekana itachukuliwa na kipa wa klabu ya Chelsea Kepa Arrizibalaga.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa