Kaze: Yanga Hii Itafuzu Makundi Ligi ya Mabingwa

HUKU wengi wakiamini Yanga SC kuanzia nyumbani katika mchezo wa hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal itawazuia kufuzu hatua ya makundi, kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze ameibuka na kushusha presha kwa kusema kikosi chao kinaweza kupata ushindi popote.

 

Kaze: Yanga Hii Itafuzu Makundi Ligi ya Mabingwa
Cedrick Kaze
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wamefuzu hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwaondosha Zalan FC ya Sudan Kusini kwa matokeo ya jumla ya mabao 9-0.

Katika hatua ya kwanza, Yanga watavaana na Al Hilal ya Sudan ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 8, mwaka huu.

 

Kaze: Yanga Hii Itafuzu Makundi Ligi ya Mabingwa

Kaze alisema: “Hatuwezi kusema mchezo wetu uliopita dhidi ya Zalan ulikuwa kipimo sahihi katika mashindano haya, ni kweli tunawaheshimu tumezungumza na wachezaji wetu kuwakumbusha juu ya hilo, kuhakikisha wanasahau matokeo ya michezo iliyopita na kuanza upya, tutaanzia nyumbani katika mchezo huu, lakini kwa ubora wa kikosi tulichonacho tunaamini tunaweza kupata matokeo mazuri popote na kufuzu hatua inayofuata.”

 

Kaze: Yanga Hii Itafuzu Makundi Ligi ya Mabingwa

Baada ya mchezo huo wa nyumbani, Yanga itaenda Sudan kurudiana na Al Hilal, mechi ikipangwa kuchezwa kati ya Oktoba 14-16, mwaka huu ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi.

Acha ujumbe