Kocha Mkuu wa Ihefu, Juma Mwambusi amesema kuwa kwa sasa ameendelea kufanya maboresho katika kikosi chao ili kupunguza mapungufu kadhaa.

Akizungumzia maandalizi yao Mwambusi alisema: “Kikosi kimerejea mazoezini kwa ajili ya kujiandaa na michezo mingine ya ligi.

“Katika mchezo uliopita tuliruhusu bao lakini hiyo ni kutokana na makosa aliyofanya kipa kwa kutokuwa sehemu sahihi.

“Nipo kwenye kiwanja cha mazoezi kwa ajili ya kufanya marekebisho ya yale makosa niliyoyaona pia kuongeza yale mazuri zaidi ili timu iwe bora.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa