Stori nyingine inayozungumzwa na wachambuzi wengi wa michezo nchini ni juu ya uwezo wa kawaida wa magolikipa wakigeni ambao wanacheza kwenye klabu za ligi kuu.

Kipa wa zamani wa Yanga na KMC anayekipiga kwenye klabu ya Mtibwa Sugar Faruk Waza Shikhalo ni moja ya wahanga wa uchambuzi huo, baada ya kufungwa mabao matatu akiwa langoni wakati Azam FC wakishinda mabao 4-3 wikiendi iliyopita.

Yanga, Kipa wa Yanga Alipagawa Golini, Meridianbet

Faruk hakumaliza mchezo huo kwani alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kipa mwingine ambaye aliruhusu bao moja. Kocha wa timu hiyo Salumu Mayanga ameibuka na kusema kuwa Faruk hakuwa sawa tena baada ya kufungwa mabao yale matatu.

Mayanga alisema: “Baada ya kuruhusu magoli matatu hakuwa sawa tena kiakili ilikuwa ni lazima nimfanyie mabadiliko na kumuingiza kijana mdogo.

“Nakiri kwamba nina shida sana kwenye eneo la nyuma na nahitaji nguvu, nashukuru waliokuwa majeruhi wameanza kurejea bila shaka mechi inayofuata nitaimarika.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa