Clement Mziza ndiyo mchezaji aliyepeleka kilio kwa Kagera Sugar wilkiendi iliyopita wakati Yanga Sc walipoilaza Kagera Sugar kwa baoa 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Mziza, amefunguka kuwa mbali ya Feisal Salumu kutoa pasi ambayo ilimpa nafasi yeye kufunga, kuna wachezaji wengine akiwemo straika Fiston Mayele ambaye alimpa nguvu na kumtia moyo kuwa ni muda wake umefika wa kuipandia timu yake.
Mziza ni kinda aliyeipandishwa kutoka kwenye kikosi cha U20 na mchezo wa juzi ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, huku zile zingine aliingia akitokea benchi.
“Nashukuru sana Mungu kwa kuweza kufunga bao langu la kwanza ndani ya Yanga na kuweza kuisaidia timu yangu kupata pointi tatu muhimu. Nishukuru pia kaka zangu na wachezaji wenzangu akiwemo Mayele.
“Nilipopewa nafasi ya kuaza kwenye mchezo huo, Mayele aliniambia nisiwe na wasiwasi nijiamini na nionyeshe kile ninachofanyaga kwenye uwanja wa mazoezi. Kina Kibwana Shomari, Yusuf Athuman na wengine walinipa moyo sana,” alisema.