Mchezaji wa Shakhtar Donetsk Mykhaylo Mudryk amesema kuwa anaifuatilia Arsenal kwa karibu huku kukiwa na uvumi kuhusu uwezekano wa kuhamia The Gunners dirisha dogo la usajili Januari.
Mchezaji huyo ameonyesha kiwango cha kuvutia msimu huu ambapo kimemfanya Mudryk awavutie Arsenal ya Arteta msimu huu huku akihusika na mabao 16 katika mechi nyingi na kuvutia baadhi ya vilabu vya juu vya Uropa, huku mchezaji huyo wa miaka 21 akihusishwa kwa karibu na Arsenal.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ukraine anasema ameendelea kutazama kwa ukaribu kiwango cha kuvutia cha The Gunners, ambacho kinawafanya wabaki kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi tano kuelekea mapumziko ya Kombe la Dunia.
Alisema kuwa; “Ninaziangalia kwenye ‘MyScore’ na kujua zinapocheza naweza kuziangalia, mimi pia huwatazama. Ni timu yenye nguvu sana, kwa ujumla sio tu katika kudhibiti mpira lakini pia katika kufunga mabao.”
Hata hivyo, Mudryk angetaka kuhakikishiwa kuhusu muda wake wa kucheza kutoka kwa kocha wa Arsenal Mikel Arteta na kusema kuwa anataka kujua kwanza kutoka kwa kocha mkuu kwamba angepata nafasi katika kikosi.
Huku akiongezea kusema kuwa anachotaka kusikia moja kwa moja kutoka kwa Arteta ni jukumu lake kuwa upande wake na kwa mtazamo wa dhahania kama kungekuwa na chaguo la kuwa mchezaji wa benchi kwa Real Madrid au kuanza kwa Arsenal, labda huenda angechagua kwenda The Gunners.
Mudryk aliripotiwa kukaribia kuondoka Shakhtar katika dirisha la usajili lililopita, lakini akaishia kusalia na mabingwa hao mara 13 wa Ligi Kuu ya Ukraine.
Ingawa alisikitishwa na hatua hiyo ambayo haikufanyika, Mudryk alikiri kwamba kuchelewa kwa kuondoka kunaweza kumletea faida, akisema kuwa; “Nilizungumza na makocha wakuu wawili au watatu, Walikuwa Nice, Bayer Leverkusen na Brentford.”
Lakini iliposhindikana alifahadhaika kidogo lakini kama wanavyoona sasa mpango wa Mungu ni bora kuliko ndoto zake. Mchezaji huyo alisema.