Kocha msaidizi, Juma Mwambusi, ameomba kukaa kando kwa sasa ndani ya kikosi cha Yanga kwenye majukumu ya kuwa kocha msaidizi.
Hatua hiyo imefikia baada ya yeye mwenyewe kuandika barua baada ya kikosi hicho kutwaa taji la Mapinduzi ambapo iliifunga Simba kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana, Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kwenye barua yake ya kuomba kujiweka kando ametaja sababu kuwa ni kuwa na matatizo ya kiafya.
Ameongeza kuwa Mwambusi ameshauriwa na wataalamu kukaa sehemu ambayo itamfanya asiwe na msongo wa mawazo pamoja na kupiga kelele.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi ambaye ameachiwa jukumu la kusaka msaidizi wake.
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.
Ernest Kimeru
Yanga wameshalimwaga huku
Shakila mrope
Unakaribishwa utopolo mzee
Magdalena
Duh uyu nae anataka kukwamisha watu
Angelina
Duuh hatari
Sadick
Mwambusi ni Kocha mzuri na anatakiwa kuwa Kocha mkuu sio msaidizi wa yeyote
Adelta
Kwanza nampongeza kwa kutoa ubingwa wa mapinduzi pili mapumziki mema ya kiafya
Fatuma kasomo
Mh
David Pere
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi ambaye ameachiwa jukumu la kusaka msaidizi wake.
Sania
Mhh kuna shida hapo
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri niakilizake zimemtuma na mamuzi yake
Hopemwaikuka
Kuna jambo hapo
Dorophina
Kama ni matatizo ya kiafya sio mbaya muache apumzike amefanya kazi nzuri kwenye klabu
felister
sio mbaya
Sarah
Mh sio bure kutakuwa nashida
Venerose
Hapo kuna tatizo
Rahmal
Duuh atali apo akupo saw kuna namna
Tatu
Sio mbaya
Issa
Asepe tu
warda
Wesha anza kutibuana