Klabu ya Yanga imerejea Dar-Es-Salaam baada ya kutoka kuchukua pointi 3 muhimu dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC uliofanyika huko Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.

 

Yanga Yarejea Dar-Es Salaam Kujiandaa na Mchezo wa Shirikisho

Yanga ilichukua pointi 3 baada ya kushinda kwa bao 1-0 ambalo walilifunga kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mchezaji wao Bernard Morrison katika kipindi cha kwanza na hatimaye kusalia kileleni kwa msimamo wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 20.

Na sasa Young Africans wanajiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Barani Africa, baada ya kutolewa katika michuano ya Klabu Bingwa huku mechi hiyo ikitarajiwa kupigwa siku ya Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga Yarejea Dar-Es Salaam Kujiandaa na Mchezo wa Shirikisho

Africain wamefika hatua hiyo baada ya kumtoa Kipanga anayeshiriki ligi ya Zanzibar. Hatua hiyo ni ya mtoano na mechi ya marudiano itakuwa ni kule Tunisia tarehe 9 na mshindi kati yao ndiye atakayetinga kwenye hatua ya makundi.

Club Africain wao wameshatua Tanzania rasmi kujiandaa na mchezo huo, huku kwa upande wa Yanga wao kupitia Rais wa klabu hiyo Hersi Said akisema kuwa wamejiandaa vizuri kukabiliana na Watunisia hao na wanahitaji kutinga hatua ya makundi.

Yanga Yarejea Dar-Es Salaam Kujiandaa na Mchezo wa Shirikisho

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa