Harry Maguire ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi kuliko mwanasoka yeyote kwa mwaka 2020. Takwimu mpya zinaonesha kuwa Harry amecheza dakika nyingi kuliko mchezaji yeyote wa kulipwa, ikiwa ni pamoja na kuwazidi magolikipa.
Nahodha huyo wa Manchester united amekuwepo uwanjani kwa jumla ya dakika 4,745 ambazo ni zaidi ya masaa 79 kwa mwaka huu tu hadi Disemba 17. Hii ni kwa mujibu wa takwimu kutoka CIES Football Observatory.
Maguire amewaacha Ruben Dias wa Man city, nahodha wa Barca Lionel Messi na mchezaji mwenzake wa Man united Bruno Fernandes ambao ni wachezaji wanaocheza namba za ndani walioingia katika orodha hiyo. Pamoja na hivyo bado Maguire amecheza dakika tano (5) zaidi ya mlinda mlango namba moja wa Internacional ya Brazil, Marcelo Lomba.
Maguire hajakosa mchezo wa Epl akiwa na Man U tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Leicester city kwa dau la £80 majira ya joto mwaka 2019.
Mchezaji Timu Dakika
1. Harry Maguire Man Utd 4745
2. Ruben Dias Man City 4344
3. Lionel Messi Barcelona 4293
4. Bruno Fernandez Man Utd 4164
5. Bruno Pacheco Ceara 4162
6. Romelu Lukaku Inter 4144
7. Victor Lindelof Man Utd 4142
8. Raphael Varane Real Madrid 4123
9. Jesus Navas Sevilla 4110
10.Callum McGregor Celtic 4106
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???
Maguire ni mchezaji makini Sana
Maguire ni mchezaji mzuri sana
Safi sanaaa
Safi
Safi
Safi
Maguire moto united
Imeeleweka
Safi sana
Safi sana
Safi
Safiii Sana majukumu yake yakaz nakujituma pia
Hongera yake
Binafsi nina mashaka na Maguire kwenye maamuzi yake uwanjani lakini anaonyesha kuwa kiongozi mzuri kwa wenzake