Msimu mpya wa NBA umefungulia usiku wa kuamkia leo. LA Lakers walikuwa uwanjani kupambana na LA Clippers wakati ambapo Brooklyn Nets walichuana na Golden State Warriors.
Lakers walijukuta wakipoteza mchezo dhidi ya Clippers baada ya kumaliza mchezo kwa pointi 109-116. Alikuwa ni Paul George aliyeng’ara kwenye mchezo huo baada ya kuipatia Clippers pointi 33 kabla ya Kawhi Leonard kuongeza zingine 22 katika kipindi cha pili.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa LA Clippers kushinda mechi ya kwanza kwenye misimu ya NBA.

Upande wa pili, Kevin Durant aliiongoza Brooklyn Nets kwenye mchezo dhidi ya timu yake ya zamani – Golden State Warriors.
KD alijiunga na Nets kwa mkataba wa miaka 4 akitokea Warriors 2019. Licha ya kutoitumikia Nets kwa sehemu kubwa ya msimu uliopita baada ya kupata majeruhi, KD aliisaidia Nets kuibuka na ushindi wa pointi 125-99.
Durant alipachika pointi 22 wakati ambapo mpinzani wake Stephen Curry aliisaidia Warrior kupata pointi 20 na alitoa pasi 10 za magoli.

Akizungumzia kurejea kwa KD kwenye msimu huu wa NBA, kocha wa Brooklyn Nets – Steve Nash alisema, “Kuna tofauti kubwa sana ya kuwa nje ya NBA kwa miezi 18 na ukarejea tena baada ya yote aliyoyapitia.
“Anaonekana kama Kevin, anacheza kama Kevin lakini sitaki kuweka matarajio yangu kwake mpaka pale atakapokuwa vizuri zaidi na atakapozoea kucheza mechi 3 ndani ya siku 4.
“Kwake ndio hatua inayofuata. Tunapaswa kumtizama siku baada ya siku.”

Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza, kama ilivyodesturi ya mashindano hayo – bingwa watetezi [LA Lakers] walikabidhiwa pete zao za ubingwa kabla ya mchezo.
Pete za Lakers zimeweka picha ya Mamba kama sehemu ya kumuenzi gwiji wa timu hiyo – Kobe Bryant ambaye alifariki kwa ajali ya chopa mapema mwezi Januari.
Pete hiyo pia imewekwa namba 8 na 24 zikiwa ni namba za jezi alizowahi kuzitumia Bryant wakati alipokuwa na timu hiyo pamoja na kuwekwa nakshi ya jezi ambazo zimestaafishwa na timu hiyo.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



Adelta
Kevin yuko vizuri ila aongeze juhudi
Caroline
Lakers mmeniangusha chama langu
Angelina
Lakers nilitegemea ushindi
Sarah
Lakers mmeharibu Kila kitu
Magdalena
Lakers wanakwama wapi
Rahmal
Nic
Issa
Lakers wameanza kupotea
Hopemwaikuka
Ilkua siku mbaya kwa lakers
Saupha mohamed
Lakers mmezingua sana
Tatu
Lakers wanakwama wapi
Mwanahamisi
Nice
Lydia Emmanuel Magoti
Haikuwa kazi laisi kwao Lakers
warda
Huwezi kuwa juu kila siku
Ernest Kimeru
Sio mbaya mwanzo mgumu