Hatimaye Real Madrid imemtangaza rasmi David Alaba kama mali yao baada ya rais Perez kumkabidhi mchezaji huyo jezi yenye namba 4 mgongoni.
“Ninayo furaha kubwa kuvaa jezi nyeupe ya Real Madrid, nitajituma na kutoa kila kitu nilichonacho ili klabu yetu ifanikiwe”, alisema David Alaba
David amekabidhiwa rasmi jezi namba 4 iliyokuwa ikivaliwa na Sergio Ramos. Ikumbukwe pia Hispania sheria ya namba za jezi ni 1-25.
Alaba anacheza nafasi ya beki wa kati huku akitumia mguu wa kushoto na katika michuano ya Euro 2020 akiwa na Austria alicheza mechi nne na kutoa pasi mbili za magoli.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!



Sarah
Alaba Yuko vizuri