Antony, Martial, Mctominay Kuikosa Barcelona

Wachezaji wa klabu ya Manchester United Antony, Anthony Martial na Scott ,ctominay wanaelezwa wako kwenye nafasi kubwa ya kuukosa mchezo wa kombe la Europa dhidi ya klabu ya Barcelona.

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag wakati anazungumz ana waandishi habari alilulizwa kuhusu kurejea kwa wachezaji hao katika mtanange dhidi ya Barcelona Alhamisi ijayo na kusema hana uhakika kwa aslimia 100 lakini alisisitiza hatarajii hilo kutokea.antonyKlabu ya Manchester United imeanza kuandamwa na majeruhi kwani kama mwezi mmoja nyuma aliumia kiungo wake Donny Van De Beek na kukosekana kwa msimu mzima uliobakia, Lakini siku chache zilizopita aliumia kiungo Christian Eriksen ambae atakua nje kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu, Lakini pia wachezaji kama Antony, Martial, na Mctominay wamekua wakiandamwa na majeraha ya hapa na pale.

Mchezaji Antony yeye alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi ilyomalizika dhidi ya Crystal Palace ambapo Man United waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja, Lakini Martial na Mctominay wao waliumia siku kadhaa nyuma na wataendelea kukosekana katika michezo inayofuata.antonyKocha Te Hag anatarajiwa wachezaji wake Antony, Martial, Mctominay wanaweza kuwepo nje ya uwanja kwa wiki moja zaidi. Lakini taarifa ya kufurahisha kwa mashabiki wa Man United ni kurejea kwa winga wao matata Jadon Sancho ambaye anaonekana kama amerejesha ubora wake baada ya kukosekana kwa muda mrefu ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.