Klabu ya Arsenal dhidi ya Manchester United zinashuka dimbani leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mchezo utakaopigwa katika dimba la Emirates, Huku ukitazamiwa kama mchezo mkali na wenye mvuto mkubwa baada ya miaka mingi kupita.
Vilabu vya Arsenal na Manchester United kwa miaka ya karibuni mchezo wao ulipoteza ladha na ushindani kwa kiwango kikubwa kutokana na kushuka kwa ubora baina ya timu zote mbili, Na dio jambo lililosababisha mchezo huo kukosa mvuto kama ambavyo ilikua hapo kabla.
Mchezo ambao ulivikutanisha vilabu hivo miaka iliyopita ulikua mchezo mgumu kwelikweli kwani vilabu vyote vilikua vina ubora wa hali ya juu kuanzia wachezaji mpaka makocha wa timu zote mbili, Kutokana na vigezo hivi ilipelekea mchezo kua mgumu, mvuto, na wenye ushindani wa hali ya juu.
Kocha Sir Alex Ferguson na Arse Wenger walikua moja ya vivutio vikubwa katika mchezo huo kwani walikua ni makocha hodari na wenye mbinu bora, Hivo walizitengeneza timu zao kua shidani kwa kiwango kikubwa na pale ambapo zilikua zinakuatana timu hizo basi dunia ilikua ikisimama kwa muda wa dakika 90 ili kuupisha mchezo huo.
Swali linakuja je makocha wasasa ambao wanaonekana kuzirudisha timu hizo kwenye ubora wataweza kurudisha zama ambazo mchezo huo ulikua ni moja ya michezo bora kabisa ya mpira wa miguu kutokana na ubora wa timu zote mbili. Erik Ten Hag na Mikel Arteta wanaonesha kila dalili ya kurudisha zama za ubora wa vilabu hivo.
Arsenal mpaka sasa wanaongoza ligi kuu ya Uingereza kwa tofauti ya alama tano na nafasi ya pili klabu ya Manchester City na wameonesha ubora mkubwa sana ndani ya msimu huu, Huku Manchester United wao wakiwa nafasi ya nne lakini kocha Erik Ten Hag anaonekana kuijenga timu hiyo na kua moja ya timu shindani kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

