Vinara wa Ligi kuu ya Uingereza Arsenal sasa wamehamia kwenye kumsajili mchezaji wa Brighton Leandro Trossard kwenye dirisha hili dogo la usajili huku mazungumzo tayari yameanza kwa pande zote mbili.

Ofa rasmi kwa mchezaji huyo itakuwa ni mkataba wa kudumu kusalia hapo Emirates huku Trossard akiwa hakucheza mechi iliyopita ya Brighton waliyoshinda dhidi ya Liverpool kwa mabao matatu bila.
Masharti binafsi kati ya Arsenal na mchezaji tayari yameshakubaliwa na yataendelea kwaajili ya mchezaji huyo hatari kutia saini mkataba ndani ya kikosi cha Mikel Arteta.
Arsenal ya Arteta wanawazidi Manchester City ambao wapo nafasi ya pili pointi 8 pekee huku timu hiyo ikitarajia kushuka dimbani leo dhidi ya vijana wa Conte Spurs kwaajili ya kusaka pointi 3 ambazo walizopoteza mechi iliyopita.

The Gunners wanautaka ubingwa wa EPL ambao hawajaupata kwa muda mrefu na kucheza pia Ligi ya Mabingwa ambayo pia imekuwa kama ndoto kwao. Lakini je wataweza kuhimili kushikilia nafasi hiyo licha ya kuwa mbele pointi nane?

