Arteta: Akili Yangu Ipo Arsenal

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amesema akili yake kwasasa ipo ndani ya klabu ya Arsenal ameyazungumza hayo baada ya kuulizwa kuhusu kujiunga na klabu ya Real Madrid.

Kocha Arteta ameanza kuhusishwa na kuchukua mikoba ya kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ambaye anaonekana kutofanya vizuri na klabu hiyo kwasasa, Lakini kocha huyo wa Arsenal alipoulizwa kuhusu jambo hilo alisisitiza kua akili yake kwasasa ameiweka ndani ya klabu ya Arsenal.ArtetaKocha Mikel Arteta ameendelea kusisitiza kua ana furaha ndani ya klabu ya Arsenal na anajivunia kuwepo ndani ya klabu hiyo, Kocha huyo amekua na msimu mzuri ndani ya klabu ya Arsenal kwani ameiwezesha klabu hiyo kuongoza ligi mpaka wakati huu huku wakionekana kama klabu inayopewa nafasi zaidi kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Real Madrid kwasasa inaelezwa inatafuta kocha wa kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti ambaye anaonekana kutokufanya vizuri msimu huu, Na miongoni mwa makocha wanaotajwa kuchukua nafasi ndani ya klabu hiyo ni kocha wa klabu ya Arsenal ambaye amekanusha kujiunga na timu hiyo.ArtetaKocha Arteta amefanikiwa kuijenga klabu ya Arsenal kwa kipindi cha miaka minne mpaka sasa inaonekana moja ya timu tishio ndani ya ligi kuu ya Uingereza, Jambo ambalo limefanya klabu kubwa kama Real Madrid kuvutiwa nae kutokana na uwezo ambao ameuonesha ndani ya Arsenal.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.