Baada ya kufunga bao la ushindi hapo jana dhidi ya Wolves, meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amemsifia mshambuliaji wake Lacazzete na kusema anacheza na kujituma kama vile ana malengo ya kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo.

 

arteta, Arteta : Lacazette ana Malengo na Arsenal., Meridianbet

Arteta anasisitiza kuwa nahodha Alexandre Lacazette anajituma kama mtu anayetaka kubaki Arsenal baada ya Mfaransa huyo kuwaongoza The Gunners kupata ushindi wa 2-1 wa dakika za lala salama dhidi ya Wolves.

The Gunners walionekana kukaribia kupoteza katika mbio za kumaliza katika nne bora lakini hatimaye wakatoka washindi 2-1 huku Jose Sa akijifunga baada ya juhudi za Lacazette kwenye nyavu zake katika dakika za mwisho.

Arteta alisema: “Ninapomuona mshambuliaji wetu dakika ya 85, akimkimbiza beki wa pembeni kwenye kibendera cha kona, akachukua mpira, anacheza, anaenda, anapigana, anapoteza nafasi moja, anakosa nafasi mbili, ana kwenda tena, nifanye nini.?

“Ninaweza tu kumsifu na kujaribu kumsaidia kadri niwezavyo na kumpa sapoti. Mwisho alipata matokeo. Kwangu mimi, ni bao la Lacazette.” aliongeza Arteta.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa