Aubameyang Anyemelewa na PSG

Paris Saint-Germain wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang wa Chelsea msimu wa dirisha dogo linaloanza Januari, na mchezaji huyo mpaka sasa ana miaka 33.

 

Aubameyang Anyemelewa na PSG

Aubameyang  alijiunga na Blues msimu huu wa dirisha kubwa baada ya miezi saba tuu kuondoka Arsenal na kwenda kujiunga Barcelona katika dirisha la usajili la Januari. Ripoti kutoka Ufaransa zinasema kuwa tayari mazungumzo yanaendelea kuhusu mchezaji huyo kuhamia kwa wababe hao wa Ligue 1 msimu ujao wa joto.

Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon anaanza kupata muunganiko mzuri ndani ya Chelsea huku akifunga mabao yake katika mechi zake mbili za hivi karibuni dhidi ya Crystal Palace na AC Milan.

Aubameyang Anyemelewa na PSG

Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal alisajiliwa katika  dakika za mwisho, huku kocha wa zamani Thomas Tuchel akidhaniwa kuwa ndiye aliyehusika na uhamisho wa mshambuliaji huyo. Mjerumani huyo ambaye alimpisha Graham Potter ambaye huenda akaunga mkono maono ya Boehly kwa kutenegeneza  kikosi cha vijana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.