Mabosi wa Azam wanaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars raia wa Ivory Coast, Idriss Diomande, baada ya nyota huyo aliyehusishwa pia kuhitajika na Simba katika dirisha hili dogo dili lake kugonga mwamba.
Nyota huyo alikuwa akihusishwa kujiunga na Simba kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kiungo mshambuliaji, Jean Charles Ahoua aliyejiunga na CR Belouizdad ya Algeria, ingawa baada ya Clatous Chama kurejea kikosini hapo, dili lake limeota mbawa.
Baada ya Chama kurejea Simba, uongozi wa Azam umefungua rasmi mazungumzo ya kumuhitaji kiungo huyo aliyejiunga na Singida Black Stars Agosti 20, 2025, akitokea Zoman FC ya kwao Ivory Coast, huku akisaini mkataba wa miaka mitatu hadi Juni 30, 2028.


