Ligi Kuu ya NBC Tanzania Yapanda Chati za Dunia

Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, imeendelea kuthibitisha hadhi yake barani Afrika baada ya kutajwa rasmi miongoni mwa Ligi 10 Bora kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS). Kwa takwimu zilizotangazwa hii leo, Ligi Kuu ya NBC imeorodheshwa nafasi ya sita (6) kwa ubora barani Afrika, huku ikishika nafasi ya 54 duniani.

Kwa upande wa Afrika, Ligi Kuu ya NBC imeshuka kwa nafasi mbili ikilinganishwa na mwaka 2024, lakini bado imeendelea kusalia ndani ya orodha ya ligi bora zaidi barani humo. Hata hivyo, kimataifa Ligi hiyo imepiga hatua kubwa kwa kupanda nafasi tatu duniani, kutoka nafasi ya 57 mwaka 2024 hadi nafasi ya 54 mwaka 2025.

Ligi Kuu ya NBC Tanzania Yapanda Chati za Dunia

Kupanda huko kumeambatana na ongezeko la alama, ambapo Ligi Kuu ya NBC imeongeza pointi kutoka 266.75 mwaka 2024 hadi kufikia 308.5 mwaka 2025. Ongezeko hilo linaakisi maendeleo yanayoendelea kufanywa katika ushindani, uendeshaji wa ligi, pamoja na mvuto wa soka la Tanzania kwenye majukwaa ya kimataifa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa shukrani zake kwa wadau wote wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwemo klabu, wachezaji, waamuzi, wadhamini na mashabiki, kwa mchango wao mkubwa ulioifanya ligi hiyo kuendelea kuwa miongoni mwa ligi bora na zenye mvuto mkubwa barani Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.