Chama Ana Imani Kubwa Na Simba Yake

Ikiwa ni masaa machache yamepita tangu urejeo wa kipenzi cha wanasimba, Clatous Chama, mwenyewe ameibuka na kauli nzito na yenye kutia Imani kwa mashabiki alipozungumza mara ya kwanza baada ya kutambulishwa na wekundu hao wa Msimbazi.

Licha ya Simba kutokuwa na mwanzo mzuri wa msimu, kiungo huyo mshambuliaji mwenye rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye mashindano ya kimataifa, amesema bado hakuna sababu ya kukata tamaa amesisitiza kuwa muda upo kwa timu hiyo kuamka na kusonga mbele na kurejea tena kwenye utawala wa soka la  Tanzania na Afrika.

Chama Ana Imani Kubwa Na Simba Yake

Chama amesema matokeo yasiyoridhisha waliyoyapata Simba katika michezo ya awali haipaswi kuwavunja moyo wachezaji, kwani bado msimu una safari ndefu na nafasi ya kurekebisha makosa ipo wazi.

“Matarajio ya msimu hayajatimia kwa matokeo yaliyopatikana kwenye mechi za mwanzo mwa msimu huu, sio mazuri, lakini muda bado upo. Hatujachelewa, tutaamka na kufanya kazi, na mwisho wa msimu tutakuwa na furaha,” amesema Chama.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ameeleza kuwa kilicho muhimu kwa sasa ni kuongeza nguvu, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wachezaji ili kupambana kwa ajili ya nembo ya Simba na kufanikisha malengo waliyojiwekea.

Chama amesisitiza kuwa ana imani kubwa na kikosi kilichopo, akiamini kuwa kwa bidii, nidhamu na kujituma, Simba itaweza kurejea kwenye mstari na kuonyesha kiwango kinachotarajiwa na mashabiki wake.

Chama Ana Imani Kubwa Na Simba Yake

Akizungumzia kurejea kwake ndani ya kikosi, Chama amesema anafahamu matarajio makubwa ya mashabiki wa Simba, jambo linalompa motisha ya kuongeza juhudi, nidhamu na kujitoa kwa hali na mali ili kuisaidia timu kufikia malengo ya msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.