David Beckham anaamini kucheza na kuiunga mkono Uingereza ni fursa mwafaka kwa wachezaji na mashabiki kusherekea maisha ya Malkia Elizabeth ΙΙ aliyefariki wiki iliyopita huko Uingereza.

 

Beckham: Mpira wa Miguu Kusherehekea Maisha ya Malkia

Malkia ambaye alikuwa ametawala nchini Uingereza kwa miaka 70 akiwa na miaka 96 mnamo Septemba 8. Wakati Taifa likiingia kwa siku 10 za maombolezo ya Kitaifa, Chama cha Soka cha (FA) kilitangaza kuahirisha mechi zote kuanzia ligi za mpira na na michezo mingine.

Hiyo ni pamoja na mechi 10 za  ligi kuu ya Uingereza zilizopangwa kuchezwa wiki iliyopita, huku michezo saba pekee ya ligi kuu itafanyika wiki hii  kutokana na masuala yanayohusisha vifaa vya mazishi ya mfalme, yatakayofanyika London Septemba 19.

Beckham ambayee ni nyota wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na England alijiunga na foleni Ijumaa, na ambapo mechi za ligi zinarejea na za Kimataifa zikikaribia nahodha huyo wa zamani wa England anatumai kuwa mchezo huo unaweza kusaidia kusherehekea maisha na utawala wa Malkia . Alisema kuwa;

 

Beckham: Mpira wa Miguu Kusherehekea Maisha ya Malkia

“Kunapaswa kuwa na heshima kila wakati kwa Malkia wetu na nchi kwa wakati huu wa maombolezo”  “Lakini kama nikizungumza kama mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu, na nahodha wa zamani wa England, najua ilimaanisha nini kwetu kutoka kwenye uwanja huo na kumwakilisha Malkia, na nchi yetu ya England.

Beckham aliongezea kwa kusema kuwa wanapokuwa nje ni fursa ya kusherehekea kwa njia ya mpira wa miguu na mashabiki wake. Uingereza itacheza na Italy Septemba 23 kabla ya kuwakaribisha Ujerumani kwenye uwanja wa Wembley siku tatu baadae kwa mchezo wao wa mwisho kabla ya Kombe la Dunia la Qatar, ambalo litaanza Novemba.

 

Beckham: Mpira wa Miguu Kusherehekea Maisha ya Malkia

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa