WAKATI Yanga wakitarajia kucheza leo jumamosi dhidi ya Zalan FC kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa.

Mchezo huo wa marudiano wa michuano ya Klabu bingwa barani utachezwa saa 1:00 usiku.
Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa kifua mbele baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza yakifungwa na Feisal Salum huku Fiston Mayele akifunga matatu.

Kupitia ukurasa wa klabu hiyo leo wamemtangaza Waziri Mchengerwa kuwa Mgeni rasmi katika mchezo huo wa marudiano.


