SEPTEMBA 17,2022 Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku ambapo kuwaona mastaa wa Yanga ikiwa ni pamoja na Farid Musa, Fiston Mayele, Feisal Salum ni buku mbili tu, (2,000).

Yanga, Kuwaona Yanga vs Zalan FC ni Buku Mbili Tu, Meridianbet

Kwa upande wa VIP A kiingilio ni 15,000, VIP B & C ni 10,000 na mzunguko ni 2,000.

Yanga itaingia ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wa awali iliposhinda mabao 4-0, Uwanja wa Mkapa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa wanatambua mchezo wao ujao utakuwa na ushindani mkubwa lakini wapo tayari na watafanya maandalizi mazuri.

“Maandalizi mazuri yanahitajika kwa ajili ya mchezo wetu ujao wa kimataifa, ambacho tunahitaji ni kusonga mbele kimataifa itawezekana kwa kila mchezaji kujituma,” amesema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa