Zlatan Ibrahimovic nyota wa klabu ya Ac Milan mabingwa wa kandanda nchini Italia ameendelea kusisitiza hawezi kustaafu mchezo huo siku za hivi karibuni.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na jarida moja nchini Italia Ibrahimovic ameendelea kushikilia kauli yake ambayo amewahi kuitoa siku za nyuma ya kua hatastaafu mpira wa miguu mpaka pale atakapoona mtu mwenye uwezo wa kufanana na yeye ndipo atakapotundika daruga zake.

ibrahimovicMchezaji huyo mwenye sifa ya ujivuni licha ya umri wake kuasogea ila abado ameendelea kuonesha kua ana uwezo wa kupambana na katika hatua za ushindani ikumbukwe mwaka huu mwezi wa kumi nyota huyo atakua anatimiza anatimiza miaka 41 ambayo kwa kawaida wachezaji wengi wanaocheza nafasi za ndani hua wameshastaafu mpira aua wengine wameenda kushuriki ligi zisiszo na ushindani mkubwa lakini nyota huyo wa kimataifa wa Sweden bado yupo kwenye ligi ya ushindani.

Mchezaji huyo ambaye anasumbuliwa na majeruhi tangu kurejea kwake katika miamba hiyo ya soka nchini Italia ila sio jambo ambalo limemfanya awaze kuachana na soka kwani anasisistiza bado yupo sana kwenye mpira wa miguu mpaka aone mwenye bora wake ndipo na yeye atastaafu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa